Tupo Nawe

Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge aweka rekodi ya kukimbia km 42 kwa saa 1:59

Eliud Kipchoge amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya dakika mbili . Raia huyo wa Kenya alikimbia muda wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindani la Ineos Challenge mjini Vienna nchini Austria siku ya Jumamosi.

Kbla ya mbio

Mashabiki wa michezo nchini Kenya na duniani wanatazama kwa makini kuona iwapo mwanariadha wa kenya bingwa wa Olimpiki mashindano ya marathon, Eliud Kipchoge, anaweza kuwa mtu wa kwanza kuwahi kukimbia kilomita 42 chini ya saa mbili.

Mwanaridha huyo bora zaidi duniani anajaribu kukimbia kwa kasi hiyo katika mashindano yanayotarajiwa kufanyika Vienna nchini Austria mwishoni mwa juma kwa kukimbia dhidi ya muda aliokimbia katika siku za nyuma.

Alimaliza mbio kwa sekundi 26 zaidi ya alivyotarajia katika jitihada ya kwanza ya kukimbia kwa muda wa saa mbili tu huko Monza – Italia.

Lakini lengo kuu katika mashindano haya maarufu “INEOS 1:59 challenge”, sio kushinda tu. Lengo lake mwanaridha huyu wa Kenya lilikuwa wazi tangu awali wakati alipotangaza kwamba anakwenda Vienna sio kushinda, bali ni kuupika muda wake wa awali.

Mwanariadha Eliud Kipchoge kuweka rekodi mpya

“Ninakwenda katika mashindano ya Vienna 2019 kudhihirisha kwamba binaadamu hana viwango. Kuuonyesha ulimwengu kwamba hakuna lisilowezekana” alisema Eliud Kipchoge wiki iliyopita akihotubia waandishi habari nchini Kenya.

Alieleza kwamba amekuwa akifanya mazoezi kwa miezi mitatu mahsusi kwa pambano hilo la INEOS 1.59 na kwamba amekuwa akikimbia kiasi ya kilomita 200 hadi 220km kwa wiki.

‘Sio kuhusu rekodi ya Dunia, ni azimio la kuweka historia na kuwatia watu moyo’ alisema Eliud.

Lakini kulifikia hilo, wanamichezo wanasema Kipchoge anahItaji kukimbia kwa kasi ya ziada ya sekundi 26 kuliko alivyokimbia katika mashindano yaliopita huko Monza.

Muda mfupi kabla ya kuondoka kueleka Vienna, Kipchoge alituma picha akiwa katika uwanja wa ndege Eldoret tayari kwa safari:

lakini kinyume na inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini na hata katika majukwaa katika mitandao ya kijamii. Eliud Kipchoge “hatokuwa anapania kuivunja rekodi yake ya dunia”.

Kipchoge ndiye anayeishikilia rekodi ya shirikisho la riadha duniani IAAF kwa muda wa saa 2:01:39 lakini amewahi kukimbia mbio za marathon kwa kasi zaidi ya hiyo.

Hiyo ni katika jitihada za awali kuupika muda huo wa saa mbili – mradi wa Nike “Breaking2”, alipofanikiwa kukimbia kwa saa 2 na sekundi 25.

Lakini rekodi ya dunia inawekwa katika masharti makali ya mashindano , na Mathew anafafanuwa kuwa mashindano hayo ya NIke na hata yajayo ya “INEOS 1:59″ yanatimiza masharti hayo.

” Yanalenga muda… inahusu mwanariadha kuupiku muda wa saa mbili, na kila kitu kimetayarishwa kuhakikisha ana fursa nzuri” anasema Kenyon.

Wakenya waonyesha upendo

Katika kudhihirisha uzito wa mashindano haya na ina maana gani kwa wakenya, baadhi wamemiminika katika mitandao ya kijamii kupitia ujumbe kama #Eliud159 #ineos159challenge na #eliudkipchoge uliotanda pakubwa Wakenya wakionyesha kumuunga mkono mwanariadha huyo katika azimio lake mwishoni mwa juma.

Mnamo Septemba 2018, Rekodi mpya ya mbio za Berlin Marathon, ilichukuliwa na mwanariadha huyo wa Kenya, Eliud Kipchoge, ambaye ni mkimbiaji wa mbio za masafa marefu kwa kasi zaidi duniani.

Bingwa wa Olimpiki wakati huo akiwa na miaka 33, aliweka muda mpya wa saa 2, dakika 1 na sekunde 39 na kuivunja rekodi ya Mkenya mwenzake Dennis Kimetto aliyeweka rekodi mpya ya dunia ya saa 2, dakika 2 na sekunde 57 mnamo mwaka 2014 katika mbio hizo za Berlin marathon.

Nyota huyo wa mbio ndefu amevunja rekodi ya mbio hizo kwa kutimka kilomita 42 kwa muda wa saa 2 dakika 1 na sekunde 40.

Hii ilikua ni mara ya tatu kwa Kipchoge kuibuka mshindi kwenye mbio hizo za Berlin marathon.

Iwapo Eliud Kipchoge atafanikiwa katika lengo lake Jumamosi hii katika mpambano huo wa “INEOS 1:59”, na kuupiku muda wake alioweka katika mashindano ya nyuma, basi atakuwa mtu wa kwanza kuwahi kukimbia mbio za marathon kwa chini ya saa mbili.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW