Fahamu

Mwanasheria Albert Msando afafanua kisheria adhabu inayomfaa Uchebe kwa kumpiga Shilole, Iwe fundisho kwa wengine (+Audio)

Mwanasheria Albert Msando afafanua kisheria kosa alilofanyiwa Shilole kwa kupigwa na mume wake Uchebe na kueleza kuwa hilo ni kosa la Jinai.

Mbali na kukemea ameeleza ni adhabu gani inafaa kuchukuliwa juu yake na watu wengine wenye tabia kama ya Uchebe ya kuwapiga wake zao, Msando ameongeza kuwa kosa la jinai kama alilofanya uchebe sio kwa watu wanaowapiga wake zao bali kwa mtu yeyote anayepiga watu kwa maana kuwa endapo utampiga mtu kwa sababu yeyote ile hilo ni kosa la jinai.

Msando pia amefafanua juu ya makosa yapi ni ya jinai kutokana na vifungu vya sheria.

Ikumbukwe Shilole alipigwa na Uchebe ingawa katika baadhi ya mahojiano Uchebe alikataa na kusema kuwa picha hizo ni za siku nyingi na kudai kuwa siku za hivi karibuni hajampiga mke wake.

Kutokana na kauli hiyo Msando amesema kuwa “Kosa la jinai halina muda. Hata kama lilifanyika miaka ya 1980! Kama lilikuwa ni kosa kisheria basi aliyetenda lazima adhabu inamuhusu. Nitashangaa kama ‘upelelezi bado unaendelea’ mpaka ikifika mwezi wa nane. Ni vyema muda akitoka jela akute kiberiti kinauzwa elfu 15 na box spanner inauzwa kama laki 6 hivi. Tuone gereji atakuwa na spanner ngapi na ghetto atawasha jiko la mchina na nini”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents