Burudani

Mwasiti kufungua mwaka na wimbo ‘Serebuka’ aelezea chanzo cha ukimya

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kutokana kubanwa na majukumu ya kampeni ya ‘Tokomeza Zero’ muimbaji wa THT, Mwasiti Almas anatarajia kuachia wimbo mpya ‘Serebuka’

mwasiti

Akizungumza na Bongo5 leo, Mwasiti amesema alikuwa kimya sana mwaka jana kutokana na kusimamia project ya elimu ‘Tokomeza zero’ iliyomfanya azunguke mikoani ili kuhamasisha.

“Kawaida yangu ni kutoa wimbo halafu nanyamaza ila kwa mwaka jana ukimya ulipitiliza kutokana na project na nyingi zilinibana kama project ya ‘Tokomeza Zero’- hii ni ya elimu ambayo ilinifanya nizunguke mikoani ila kwa mwaka huu ni kazi tu.Nimepanga nitoe nyimbo tatu au mbili nikianza na Serebuka ambayo nilipanga ije na video yake ila kuna mambo yameingiana nitaanza na audio wiki ijayo na video itafuata siku za usoni.”

“Serebuka ni wimbo ambao unazungumzia matukio mengi ya mapenzi. Sijazungumzia mtu mmoja, nimezungumzia watu wengi ambao wamekutana na vituko vingi vya mapenzi. Unashanga watu wanafumaniana lakini bado wanapendana. Kwahiyo Serebuka sio furaha peke yake unatakiwa utambue hata kama ukiachika leo na mpenzi wako utapata mwingine wala sio mwisho wa maisha,au unashanga unakaa na mtu miaka mingi ukitarajia mtaoana lakini inakuja kutokea anaoa mtu mwingine, kwahiyo hayo ni mapenzi.”

Pia Mwasiti amesema mwaka huu anatimizia miaka 8 kwenye muziki hivyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwakuwa mwaka huu utakuwa wa mapinduzi kwa muziki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents