Tupo Nawe

Mwinyi Zahera afunguka “Nimeisaidia Yanga mil 100 tangu niingie hapo, zingine nilikuwa nawakopesha wachezaji” – Video

Mwinyi Zahera afunguka "Nimeisaidia Yanga mil 100 tangu niingie hapo, zingine nilikuwa nawakopesha wachezaji" - Video

Aliowahi kuwa kocha wa klabu ya Yanga mzaliwa wa DR Congo Papa Mwinyi Zahera amefunguka mengi sana kuhusiana na maisha yake akiwa anaitumikiwa klabu ya Yanga kabla ya kutimuliwa mnamo tarehe 5 mwezi Novemba 2019.

Na hii inaelezwa kuwa sababu kubwa ya kutimuliwa Yanga ni matokea mabovu katika michuano ya Shirikisho barani Afrika baada ya kufunga michezo yote miwili na klabu ya Pyramids kutoka Cairo nchini Misri kwani katika mchezo wa kwanza uliochezewa Mwanza nchini Tanzania Yanga walipoteza kwa jumla ya goli 2-1 lakini katika mchezo wa marudiano ulichezwa Cairo Yanga walipoteza pia kwa kufungwa jumla ya goli 3-0 na matokeo hayo kupeleka Yanga kutupwa nje ya michuano hiyo.

Kocha huyo wa Zamani ya mabingwa hao wa kihistoria nchini Tanzania Dar Young African (YANGA) akiwa anafanya mahojiano na kituo cha habari cha Clouds Fm Mwinyi Zahera amesema kuwa “Nimetoa fedha zangu nyingi sana kuisaidia Yanga na zinafikia dola elfu hamsini kiasi ambacho ni sawa na Tsh milioni mia moja” na ameongeza kuwa “zingine nilikuwa nawakopesha wachezaji wakiwa bado hawalipwa mshahara au mchezaji amekutwa na matatizo labda amefiwa na mengine”

Kauli ya klabu ya Yanga ilikuwa hii siku wanamtimua Mwinyi Zahera.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW