Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Mwizi alewa baada ya kuiba

Mwanaume mmoja nchini Australia ametiwa nguvuni na maafisa wa polisi baada ya kukutwa akiwa ameiba katika nyumba moja.

Mwanaume  huyo mwenye miaka 36, alikutwa amelala kitandani  baada ya kuiba na kisha kulewa katika nyumba hiyo iliyopo Esperence, magharibi mwa nchi hiyo.

Maafisa wa polisi wameeeleza kuwa walipigiwa simu na mwenye nyumba hiyo baada ya kumkuta muhalifu huyo akiwa amelala kitandani baada ya kulewa mvinyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW