Michezo

Mzee Mwinyi atengua kauli ya ‘Tanzania kichwa cha mwendawazimu’ adai kwa sasa ni vinyozi

Baada ya kauli ya ‘Tanzania kichwa cha mwendawazimu kila mtu anaweza kujifunzia kunyoa’ kudumu kwa miaka 30, Hatimaye Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi amekiri wazi kufuta kauli hiyo.

Mzee Mwinyi

Mzee Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Simba SC dhidi ya Gendarmerie Tnale kutoka Djibouti, alifuta kauli hiyo baada ya mchezo huo kumalizika.

Nimeshuhudia mchezo mzuri na sasa nafuta lile neno kwamba Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila anaetaka kujifundisha kunyoa atunyoe sisi, sasa nyie ndio vinyozi.” alisema Mzee mwinyi kwenye mahojiano na vyombo vya Habari baada ya mchezo huo.

Klabu ya Simba jana ilifanikiwa kuwachabanga Gendarmerie Tnale goli 4-0 kwenye mchezo ambao ulikuwa wa kusisimua kwa mashabiki wa Msimbazi.

Soma zaidi – Simba SC yaonesha matumaini kwa Watanzania Kombe la Shirikisho Afrika

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents