Habari

Naibu Mkurugenzi wa IMF awasili nchini

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang amewasili nchini kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Kiongozi huyo akiwa nchini, Tao Zhang, atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu Jijini Dar ss Salaam

Aidha, Zhang atawasilisha mtazamo wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa wadau hapa nchini kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa na maendeleo endelevu, kuimarisha uchumi mkubwa (Macroeconomy) na kuwa na uchumi shirikishi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents