Habari

Nape awa mbogo Bungeni, ‘Mapendekezo haya yanakwenda kuiua CCM’ (+video)

Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema hakubaliani na mapendekezo ya serikali kufuta asilimia 65 ya fedha zinazotokana na mauzo ya korosho.

Nape ameyasema hayo leo, Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia hoja ya bajeti ya serikali, ambapo amesema kuwa mapendekezo hayo yanaenda kuia CCM Kusini.

“Dkt. Mpango ni kwambie mapendekezo haya yanakwenda kuiua CCM Kusini yataenda kutuweka mahali pa gumu sana,” amesema Nape.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandishi Stella Manyanya aliomba taarifa kwa kusema “Naomba mchangiaji asipende kila wakati anapochangia jambo lake kuwafanya wananchi hawa wa Kusini hawana uwezo wa kupima jambo na kusema kuwa Kusini wataenguliwa kwaajili ya korosho ,”

Nape “Kwanza niiombe mikoa inayolima Korosho sio Kusini tu Mikoa 17 wanayolima Korosho wamsamehe mama angu na shangazi yangu, kwasababu kwa bahati nzuri hajua analolisema tunazo takwimu mama angu inawezekana hajui za majibu tuliyopoteza Kusini kwasababu ya tatizo la kumisshandle gase katika nchi hii,” amesema Nape.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents