Burudani

Navio: Wanawake wa Kibongo wanajua kuwalea vyema wapenzi wao!

Inawezekana Navio amepata mtoto wa Kitanga aliyemwekea hiriki kwenye maji ya kuoga na huduma zingine adimu ndio maana hataki kuondoka Bongo.

10995039_946275575384495_2025972367_n

Rapper huyo ambaye yupo nchini kwa takriban wiki ya pili sasa alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV asubuhi hii ambapo mtangazaji alidai kuwa amesikia tetesi kuwa rapper huyo wa Uganda amepata msichana Tanzania ndio maana ameweka kambi.

Pasipo kukubali au kukataa, Navio alikiri kuwa anawapenda wanawake wa Tanzania kwakuwa wanajua kuwalea vyema wapenzi wao.

“Tanzanian women know how to treat their men,” alisema Navio.

Katika hatua nyingine Navio amepost picha akiwa studio na Mr Blue kuashiria kuwa kuna ngoma ya pamoja inakuja.

“Breaking bread with Mr Blue @mrbluebyser1988. I can’t imagine what’s about to happen. #History #Turnt,” ameandika.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents