Nelson Mandela atimiza miaka 94 leo


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela leo anasherehekea mwaka wa 94 wa kuzaliwa.
Rais Barack Obama wa Marekani na mke wake Michelle Obama, jana walituma salamu za pongezi kwa kiongozi huyo hodari wa Afrika Kusini na kumpongeza kwa unyenyekevu wake uliotukuka.
“Kwa niaba ya watu wa Marekani, tungependa kutoa pongezi zetu za dhati kwa siku ya kuzaliwa ya 94 ya Nelson Mandela na mwaka wa nne wa siku ya kimataifa ya Nelson Mandela,” alisema Obama kwenye maelezo yake.
“Maisha ya pekee ya Mandela na kujitoa kwake kusimamia sheria, democrasia na mapatano kumeendelea kuwa mfano kwa watu wa aina zote wanaotafuta utu, haki na uhuru.”
“Kwa kipimo chochote, Nelson Mandela amebadilisha historia, amebadilisha nchi yake, bara na dunia,’ yalisema maelezo hayo.
Michelle alikutana na Mandela June 11, 2011 alipotembelea Afrika Kusini akiwa na wanae.
Mandela, aliyekuwa rais wa Afrika Kusini kuanzia mwaka 1994-1999, alitumikia kifungo cha miaka 27 jela enzi za utawala wa kikaburu. Alistaafu siasa mwaka 2004.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents