Michezo

Neymar na wachezaji wenzake Wabrazil wamfanyia sapraizi Fred mazoezini kwa kujiunga Man United (+video)

Kiungo wa timu ya taifa ya Brazil, Frederico Rodrigues de Paula Santos maarufu kama Fred baada ya kutangazwa rasmi kusajiliwa na klabu ya Manchester United akitokea Shakhtar Donetsk, amepokelewa kwa shangwe na wachezaji wenzake wa timu ya taifa kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu ya Tottenham jijini London ambapo timu hiyo inafanyia mazoezi tangu wiki iliyopita.

Neymar na wachezaji wengine kama Paulinho ni moja ya wachezaji waliojitokeza mapema jana kwenye mazoezi kumpongeza Fred kwa kujiunga na Man United.

Fred amejiunga na Manchester United kwa ada ya usajili wa Euro milioni 52 na ni moja ya wachezaji wenye umri mdogo walioitwa kwenye kikosi cha Brazil kinachoenda kushiriki kwenye michuano ya kombe la dunia.
https://youtu.be/Q-EfVZaxCeA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents