Burudani

Ngwair: Mashoga wanatupunguzia ushindani wa kupata watoto wazuri

Rapper wa East Zoo, Albert Mangwea amesema ongezeko la mashoga wengi nchini halimuumizi kichwa kwakuwa linampunguzia ushindani wa kuwa na mademu wakali.

Akiongea na Power Jams ya East Africa Radio jana, amesema anashangaa jinsi mwanaume anavyoamua kuukaata uanaume wake na kuwa kama mwanamke.

“Angalia mila zetu za kiafrika, ukiangalia dini hazikubali kwamba mtoto wa kiume awe gay, hiyo tunajua yaani, common sense yenyewe hata mtoto mdogo si vitu vya kuelekezana lakini kuna watu wametokea sijui kama ni hulka au nini ambao huwezi kuwabadilisha pia huwezi kumurder mtu, watu wamekuwa wako hivyo, ukiangalia mila za kiafrika hadi akina mswati machief wetu walikuwa na mke zaidi ya mmoja, waislamu wanafanya hivyo, yaani wanawake wako wengi kwaajili ya wanaume sasa wanaume wengine wanapoamua kuwa kama wenyewe, wanapunguza mchuano, watoto wazuri wanatuachia tu. Kwahiyo mimi naona kama wao wamekataa kuwa wanaume, alisema Ngwair.”

Hata hivyo amesema watu wasimwelewe vibaya kuwa anaunga mkono ushoga kutokana na kauli yake.

“Sio kama naunga mkono lakini pia sababu wenyewe wameukataa uanaume wao mimi naona poa tu kwakuwa wanatuachia watoto wazuri wengi tu.”

“How come yaani mtoto wa kiume anakuwa gay. Mambo ya kuigaiga western huko. Western kitu cha kawaida. Lil Wayne alishaulizwa bana wewe ukipata mtoto wa kiume utajisikia vipi? Akasema nikipata mtoto wa kiume sitajua kama mtoto wa kiume, ntasubiri mpaka akue ndo nijue.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents