Burudani

Nick wa Pili kwa Joh Makini: I am real proud of you, una kipaji cha pekee!

Si kila ndugu waliozaliwa tumbo moja wanajivunia mafanikio ya kila mmoja!

Nikki wa Pili

Hata hivyo Joh Makini na Nick wa Pili ni ndugu wa aina yake. Pamoja na kuunda kundi moja la Weusi, ndugu hao wawili kutoka Arusha wanajivunia vipaji vyao.

Nick wa Pili amempongeza kaka yake Joh Makini kwa nominations alizozipata kwenye tuzo mwaka huu na kumwelezea kuwa ni rapper mwenye kipaji cha pekee.

“REAL PROUD OF U….UNAKIPAJI CHA PEKEE,” aliandika Nick kwenye picha ya Joh Makini aliyoiweka Instagram.

“Kila trak uliyogusa mwaka jana imepata nomination, I see me (wimbo bora wa hip hop), XO (wimbo bora wa hip hop), GERE (wimbo bora wa hiphop), Vitamini muzik, (wimbo bora wa RnB), Ni Penzi (wimbo bora wa RnB), Unanichora(wimbo bora wa RnB. Bado….upo kwenye msanii bora hip hop, mwandishi bora, kundi bora, Gere wimbo wa mwaka,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents