Burudani

Nikki wa Pili ampongeza JPM; ‘Vita ya kuvunja mfumo wa kifisadi ni hatari’

Msanii kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili, amendika ujumbe unaoandamana na harakati za Rais Dkt. John Magufuli za kupambana na wizi wa mchanga wa dhahabu ambao leo hii amepokea ripoti ya suala hilo.

Rais Dkt. John Magufuli

Kupitia mtandao wa kijamii Nikki ameandika, ‘Watanzania wanaopewa dhamana, wasipoamua kuwa waadilifu, umaskini utaandika historia tukufu kwa Tanzania, alafu kuna uhusiano gani kati ya uwekezaji na ufisadi…. maana kila kasha, wizi mkubwa utamkuta mwekezaji na wakala wake wa kitanzania (wasomi, viongozi, wafanya biashara), yaani ni kama ule uchumi wa kikoloni manufaa ni kwa makampuni ya nje na kitabaka cha watanzania wachache.

Nikki wa Pili

“Nimpongeze mkuu wa nchi kwa kuamua kupambana na ufisadi huu, ila vita ya kuvunja mfumo wa kiuchumi wa kifisadi ni hatari, kina Lumumba, Nkruma, Sankara, huko Chile, Nikaragwa, Venezuela, haiti, Iran…. viongozi hawakupona, ni vita kuu. Mungu akusimamie,” ameandika Nikki.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents