Burudani

Nikki wa Pili ataja mfumo anaotumia kuandika ngoma zake

Msanii kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka juu ya kutotumia peni na karatasi kuandika nyimbo zake.

Nikki kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM, amesema kuwa hatumii peni na karatasi katika kuandika nyimbo zake bali huwa anatumia mfumo wa kufreestlye.

“Mara nyingi huwa siandiki nyimbo zangu kwenye karatasi wala nini, huwa nina freestlye tu na idea ya ngoma huja wakati nina freestlye. Hatujaacha kufanya kazi na Nahreel, ila ni mambo ya kazi tu. Hata hivyo watu wategemee kusikia ngoma yangu na Nahreel,” amesema Nikki.

Kwa sasa rapper huyo anafanya vizuri na wimbo mpya ‘Quality Time’ aliomshirikisha G Nako.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents