Burudani

Nilimkuta Sam wa ukweli anauza matunda lakini…. – Meneja Maneno

Meneja maneno ambaye awali alikuwa akisimamia kazi za wasanii kadha akiwemo Sam wa Ukweli,Rich Mavoko na Diamond Platnumz amefunguka jinsi alivyomkuta msanii Sam wa ukweli akiwa anauza matunda.

Maneno amefunguka hayo katika kipindi cha “Bongo Fleva Top 20′ cha EA Radio kuwa alimkuta msanii huyo alinaehit na ngoma ya ‘kisiki’ kwa sasa akiwa anauza matunda lakini aligundua kipaji chake na kuamua kufanya ane kazi.

Maneno ambaye awali aliajiriwa katika kampuni ya kusambaza album za wasanii Tanzania ameeleza kuwa “Katika harakati zangu za kikazi nilimkuta Sam wa ukweli akiwa anauza matunda lakini alikuwa na kipaji, nikajakumsaidia na akaachia ile nyimbo yake ya Sina Raha, Hata kwetu wapo baada ya hapo akapata marafiki wapya wakamrubuni na mwisho wa siku kipaji chake kikafa”.

Kwa sasa Meneja Maneno anatamba na ngoma yake ya “Jasho langu ” aliyomshirikisha Dully Sykes.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents