Burudani

Nimefanya utafiti, nimegundua Tanzania ina wasanii bora Afrika – Seyi Shay

Muimbaji mrembo wa nchini Nigeria, Seyi Shay, amedai kuwa kupitia utafiti aliofanya, amegundua kuwa Tanzania ina wasanii wakali.

seyi-shay

Seyi Shay anayefanya vizuri sasa na wimbo wake, Right Now amesema hayo wakati akiongea na Diva kwenye kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM wiki iliyopita.

“Nimekuwa nikifanya utafiti wangu, nyie [Tanzania] mna wasanii bora Afrika, sidanganyi kabisa,” alisema. “Nasubiri sana siku moja wote tuweze kukutana na kufanya wimbo mmoja mkubwa wa wasanii wa Afrika,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Seyi alidai kuwa amemfollow Alikiba lakini yeye ameshindwa kumfollow na amemuomba afanye hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents