Habari

Nimetumia wikiendi kumsabahi Lissu ‘waliomshambulia wamemuumiza’ – Mh. Zitto

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa wikiendi iliyopita aliitumia kumsabahi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jijini Nairobi aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu eneo la ‘area D’ mjini Dodoma, huku akidai kuwa waliomshambulia walimuumiza mbunge huyo.

Mhe. Zitto ameyaeleza hayo kupitia mitandao yake ya kijamii ameeleza kuwa amerudi nikiwa mwenye unyenyekevu.

Ujasiri ni nini ?
Zitto Kabwe
Nimetumia wikiendi iliyopita kumsabahi ndugu Tundu Lissu jijini Nairobi. Nimerudi nikiwa mwenye unyenyekevu zaidi kwasababu ya nguvu na ujasiri ambao kaka yangu ameuonyesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali.
Si mara nyingi hapa nchini utasikia tukiongelea ujasiri. Lakini namfikiria Lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi. Najua hivyo ndivyo alivyo. Waliomshambulia wamemuumiza. Wamemuumiza kweli. Na bado wakati tuliokuwa naye amenionyesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri.
Alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu sio kitu rahisi kwa mtu yoyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha nimeumia moyo Sana kama asingesema maneno haya kwangu “tumeshinda. Tumeshashinda”.
Ujasiri ni Lissu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents