Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Video: Ninajua kwa uhakika Mh. Mtulia amenunuliwa – Mh. Kubenea

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, amesema kuwa anajua kwa uhakika kuwa Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia kuwa amenunuliwa kuhamia Chama cha Mapinduzi(CCM) baada ya kuachia ubunge na kujivua uanachama wake wa CUF na kuhamia CCM.

Kubenea ameyasema hayo Leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari  amesema haiwezekani  akaacha Ubunge wa Kinondoni akasema ana muunga mkono Rais Magufuli.

“Ninajua kwa uhakika kama Mbunge wa Kinondoni, Maulid Abdallah Mtulia amenunuliwa,  huwezi kuacha ubunge kwa hizi nilizowatajia bila kulipwa.  Maulid Mtulia amelipwa kiasi gani yeye na Mungu wangu haiwezekani akaacha Ubunge akaacha watu wake wa Kinondoni akasema tu yeye ana muunga mkono Rais Magufuli, kwasababu hata angekuwepo bungeni angeendelea na nafasi yake ya Ubunge huku akimuunga mkono Rais Magufuli hapo kuna biashara ya utumwa imefanyika ya binadamu ,” amesema Rais Magufuli

Aidha katika hatua nyingine Kubenea amesema kuwa hajawa kushudia soko la utumwa la kununua watu likifanyika “Mimi sijawahi kushudia soko la utumwa likifanyika la kununua watu lakini nimeona mkanda wa video wa Mh. Joshua Nassari  ukionyesha baadhi ya madiwani wakilipwa fedha na kuahidiwa huo nimeuona nimesiki kwa karibu tu kwamba mmoja wa viongozi wetu wa Chadema aliyekuwa Mwenyekiti wetu wa Taifa wa vijana alielipwa fedha nimesikia sina uhakika kama kweli au sio kweli.”

 

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW