NMB Bank Yaendelea Kuboresha huduma za Kibenki Karibu Yako!

NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuzindua bidhaa na huduma mbali mbali ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi.

Ili kukuwezesha kupata huduma za kibenki haraka na kwa wakati wowote, Benki ya NMB imeendelea kuelimisha wateja wake aina mbalimbali ya huduma za kibenki wanazoweza kuzipata bila ya kwenda katika tawi la NMB kupitia mpango wake maalum uitwao JISEVIE
Huduma zilizojumuishwa katika mpango huu maalum wa Jisevie ni pamoja na Huduma ya NMB mobile, Huduma ya NMB PesaFasta, Huduma ya NMB ATM na huduma ya kuweka na kutoa fedha kupitia Vodacom M-Pesa.

BABU GETTING JISEVIE

Wateja wa Benki ya NMB wakipata maelekezo  ya maboresho ya huduma kwa wateja wa NMB  (JISEVIE) kutoka  kwa Afisa wa NMB tawi la NMB House  Edith Mavura.
Wateja wa Benki ya NMB wakipata maelekezo ya maboresho ya huduma kwa wateja wa NMB (JISEVIE) kutoka kwa Afisa wa NMB tawi la NMB House Edith Mavura.

IMG_9849

Mpango huu wa kuelemisha wateja juu ya huduma mbali mbali wanazoweza kuzipata bila ya kupitia benki, yaani Jisevie unalenga katika kuendelea kutoa huduma bora zaidi , kuvutia na za haraka zaidi wakati wowote mteja anapohitaji huduma za kibenki”, alisema bwana Arjan Molenkamp, Afisa Mkuu wa Biashara ya Wateja Binafsi.

Wateja wa Benki ya NMB wakipata maelekezo ya huduma za JISEVIE kutoka  kwa Afisa wa NMB tawi la NMB  House Salvatory Mushi .Huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB mobile
Wateja wa Benki ya NMB wakipata maelekezo ya huduma za JISEVIE kutoka kwa Afisa wa NMB tawi la NMB House Salvatory Mushi .Huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB mobile

Wateja ambao wataweza kutumia moja ya huduma hizi zilizoainishwa katika mpango huu wa Jisevie watapata faida mbalimbali ikiwemo; kutokutumia fedha taslimu kulipia huduma mbali mbali, kuweka au kutoa fedha mahali popote kwa kutumia huduma ya Vodacom Mpesa, Kutuma fedha kwa mtu yeyote asiye na akaunti wala kadi ya ATM ya NMB kwa kutumia NMB PesaFasta na kutohitaji kutembelea tawi lolote la benki ya NMB ili kuweka fedha kwenye akaunti yako.

Afisa wa NMB tawi la Loliondo Lembris Lesion akimwelekeza  Mchungaji mstaafu Ambelikile Mwaisapile jinsi ya kujiunga na NMB mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB mobile .

Wateja wa NMB sasa wanaweza kupata huduma za kibenki popote walipo bila kutembelea tawi la NMB. Haya yote yametokana NMB Jisavie ambayo itamwezesha mteja wa NMB kuwa na NMB Mobile,NMB Pesa Fasta, POS,NMB ATM,Huduma ya kuweka na kutoa fedha kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda M-Pesa na M-Pesa kwenda Akaunti ya NMB,Zaidi ya hayo yote NMB inalenga kumuwezesha Mteja wake aweze kujihudumia mwenyewe bila kufika kwenye tawi la NMB.

Faida nyingine anazoweza kupata Mteja wa NMB kwa kupitia mpango huu wa Jisevie ni pamoja na kuangalia salio la akaunti yako, kupata taarifa fupi ya matumizi ya akaunti yako, kununua Luku,Kulipa ankra ya Maji-DAWASCO, kulipia bili ya King’amuzi ya DStv, Kulipia kodi za Mapato na kununua muda wa hewani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents