Habari

NMB yakabidhi vitanda 15 vyenye thamani ya milioni 45 kwa ajili ya chumba cha ICU cha watoto hospitali ya Muhimbili

Katika kutambua afya ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya jamii, Benki ya NMB imekabidhi vitanda 15 vyenye jumla ya thamani ya milioni 45 kwa ajili ya chumba cha watoto wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) katika hospitali za Muhimbili na Mloganzila za jijini Dar es Salaam.

Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Juma Kimori akimkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu masada wa vitanda 15 kwa ajili ya chumba cha watoto wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum(ICU) katika hospitali za Muhimbili na Mloganzila za jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi msaada huo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa NMB, Juma Kimori, alibainisha kwamba thamani ya vitanda vyote ni Sh. Milioni 45 huku akifafanua kuwa kitanda kimoja cha ICU ya watoto kimegharimu Sh. Milioni 7.5 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali kuboresha sekta ya afya.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona, aliishukuru na kuipongeza NMB kwa msaada huo na kuiomba iendelee kutoa msaada zaidi kwa ajili ya chumba hicho maalum kwa watoto.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu na Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Juma Kimori wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao kutoka hospitali za Muhimbili na Mloganzila.

“Tulipeleka maombi NMB na wametujibu hatuchoki, tunaendelea kuwaomba mtushike tena mkono, maana mahitaji ya vitanda katika chumba hicho muhimu cha kuokoa maisha ya watoto ni mkubwa, bado tunahitaji vingine saba mkiguswa tena mtukumbuke.

“Kabla ya wodi hii kuanza watoto walikuwa wanachanganywa kwenye ICU za wakubwa na kule vitanda sio sawa na hivi tulivyopokea vya NMB hata sisi wahudumu hatupati tabu sana kuvinyanyua wala mgonjwa haumii kila kitu kinasetiwa kwenye umeme asanteni sana NMB,” alisema Mawona aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.

#NMBKaribuYako

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents