Michezo

Novak Djokovic amchakaza Rafael Nadal kwenye fainali ya michuano ya Australian Open 2019

Msebia Novak Djokovic ameibuka kuwa bingwa wa michuano ya tenisi ya Australian Open 2019 kwa kumchakaza Rafael Nadal seti
6-3,6-2,6-3 .

Mhispania Rafael Nadal amechakazwa kwenye seti zote na fainali hiyo ilidumu kwa muda wa masaa wawili na dakika nne.

Katika rekodi Novak anakuwa mchezaji wa kwanza wa kiume kuchukua ubingwa wa Australian Open mara 7, akiwa mbele ya Roy Emerson na Roger Federer ambao kila mmoja amechukua mara 6.

Novak kwa sasa ndiye mchezaji wa tenesi namba 1 duniani kwa ubora kwa upande wa wanaume, na ushindi huo unamfanya kufikisha mataji 15 katika maisha yake ya mchezo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents