Michezo

Ole Gunnar atema cheche baada ya Pogba kutukanwa mitandaoni kisa kukosa penati”Lazima tufanye jambo kuhusu hili, maafisa husika lazima walishughulikie”

Ole Gunnar atema cheche baada ya Pogba kutukanwa mitandaoni "Lazima tufanye jambo kuhusu hili, maafisa husika lazima walishughulikie"

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema makampuni ya mitandao ya kijamii ni lazima yasimamie kusambaa kwa chuki baada ya mchezaji wake kiungo wa kati Paul Pogba kukabiliwa na ubaguzi katika mitandao wiki iliyopita.

Raia huyo wa Ufaransa amekuwa mchezaji wa tatu katika wiki moja kukabiliwa na ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii baada ya kukosa kufunga bao la penalti katika mechi dhidi ya Wolves.

“Paul ni kijana mahiri – inamfanya kuwa mkakamavu zaidi,” amesema raia huyo wa Norway.

“Ni lazima tufanye jambo kuhusu hili na maafisa husika ni lazima walishughulikie.”

Manchester United midfielder Paul PogbaHaki miliki ya pichaPA MEDIA

Solskjaer ndio mtu wa hivi karibuni kutoka klabu hiyo kuitisha hatua kali zichukuliwe baada ya mlinzi Harry Maguire na mshambuliaji Marcus Rashford na  Aliyekuwa mlinzi wa klabu hiyo Phil Neville wakipendekeza kuwa wachezaji wajitoe katika mitandao ya kijami kama njia ya kulalamika yaliotokea.

Harry Maguire alisema

“Mitandao ya kijamii ni sehemu ambayo watu hujificha kwa utambulisho bandia – sio uamuzi wangu ku kuyabadili,” ameongeza Solskjaer, ambaye pia amesema wachezaji hawatopigwa marufuku kutumia mitandao ya kijamii.

Wiki iliyopita, Chelsea ilishutumu “ujumbe wa matusi” uliomlenga Tammy Abraham baada ya kushindwa kufunga mkwaju wa penalti katika fainali ya Super Cup dhidi ya Liverpool. Alafu Jumapili, mshambuliaji wa Reading Yakou Meite alishutumu matusi ya kibaguzi dhid iyake kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuokolewa mkwaju.

Mapema wiki hii, Twitter ilibaini kuwa itakutana na wawakilishi wa United na wanaharakati wa kupambana na mashambulio ya matusi.

Manchester United manager Ole Gunnar SolskjaerHaki miliki ya pichaREX FEATURES

Hakuna vita kati ya Pogba and Rashford’

Wakati huo huo, Solskjaer amesema hatobadili sera yake ya penalti mara mbili baada ya kuhustumiwa mbinu zake alizotumia katika mechi iliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Wolves.

Solskjaer amesema: “Nina hakika mutamuona Pogba akiifungia United bao jingine tena. “Musishangazwe iwapo Marcus au Paul wakifunga bao linalofuata. Hakuna vita baina yao.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents