One The Incredible: Media zinasupport muziki na sio Hip Hop

One The Incredible

Rapper Harry Kaale aka One The Incredible amesema vyombo vya habari hususan redio na TV vinajitahidi kuusupport muziki wa Tanzania lakini sio kama inavyofanya kwa nyimbo za Hip Hop za wasanii kama yeye.

One ametoa kauli hiyo jana wakati wa ‘Kilinge’ (Cypher) kilichoandaliwa na Tamaduni Muzik na kufanyika Msasani Club jijini Dar es Salaam.

“Kwakweli media haitoi support kwa Hip Hop, inatoa support kwa muziki kwa asilimia kubwa lakini hip hop ni kwa asilimia ndogo sana,” aliimbia Bongo5.

“Lakini sio kitu cha kushangaza sababu hata nchi nyingi tu duniani hata huko Marekani, hip hop kama hip hop yaani lile jina la hip hop linabebwa na wasanii ambao ukikaa hata pale sio wanaoiwakilisha, kwahiyo ni kitu ambacho kipo. Ndio maana siku zote kunakuwa na mainstream na kunakuwa na underground, hip hop halisi ipo underground. Sababu wale ndio watu ambao wanahangaika zaidi kufanya kazi yao.”

Pamoja na One, Kilinge hicho kilikuwa na wasanii wakali wengine akiwemo Nikki Mbishi, Mansu-Li, Azma, Songa, P the MC, Maalim Nash na wengine ambao walitumia uzoefu wao kuwakosoa wasanii wachanga wa hip hop waliokuwa wakiimba kwenye cipher.

Mratibu mkuu wa Kilinge hicho ni producer Duke wa Tamaduni Muzik ambaye amesema kila Jumamosi watakuwa na kitu kama hicho ili kuvitambua vipaji vipya vya Hip Hop nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents