Burudani

Picha: Mayweather anunua saa yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2

Floyd Mayweather amefanya yake tena.. Bondia huyo bingwa wa kuchezea hela, amenunua saa ya kifahari yenye thamani ya dola milioni 1.1 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 2.

1214-floyd-mayweather-tmz-2

Ameinunua saa hiyo kwenye safari yake ya Dubai.

Mwakilishi wake ameiambia TMZ: The watch is roughly $1.1 million. This is just one of his big purchases.”

Saa hiyo ni ya chapa ya Hublot ambayo imezungushiwa almasi.

1214-subasset-floyd-mayweather-tmz-2

Inasemekana kuwa Floyd ametumia zaidi ya dola milioni 1.5 katika siku mbili alizokaa Dubai.

Hii ni mara ya pili bondia huyo ananunua saa ya thamani kubwa. Mwaka 2014 alinunua pia saa ya dola milioni moja yenye almasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents