Burudani ya Michezo Live

Picha: Mkutano wa Dkt. Mwakyembe na wasanii wa filamu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrion Mwakyembe leo Agosti 4, 2017 amekutana na wasanii wa filamu nchini katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere Dar es Salaam ambapo wamejadili changamoto zinazoikumba tasnia hiyo kwa sasa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe

Hapo jana Dkt. Mwakyembe alikutana na wasanii wa muziki na leo ikawa zamu ya wasanii wa filamu ambapo amewataka kutoiga vitu kutoka nje ya nchi huku akitolea mfano wingi wa makabila uliopo hapa nchini kuwa unaweza kutumika katika mambo mengi ya uigizaji.

Pia Dkt. Mwakyembe amewatakaa wasanii hao kubadilika ili kuendana na ukuaji wa teknolojia ili waweze kukuza kazi zao na kufika mbali zaidi ukilinganisha na sasa.

Tazama picha zaidi. 

 


Bi. Joyce G.Fissoo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzani


Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba

Musa Sakari Mratibu wa sindano la European Youth Film Competition 2017 Andreson Media

Kikundi cha sanaa kutoka TaSUBa wakitoa igizo fupi

 

 

 

Picha ya pamoja ya Waziri na Viongozi na wasanii wa filamu

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW