Habari

Picha: Spika Ndugai akutana na kiongozi wa chama cha Kikomunisti cha Urusi

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akutana na Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Urusi na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo, Komredi Gennady Zyuganov alipomtembelea leo ofisini kwake katika maadhimisho ya miaka 100 ya Mapinduzi Makuu ya Urusi.


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akivishwa nishani maalum ya maadhimisho ya miaka 100 ya Mapinduzi Makuu ya Urusi na Kiongozi wa Chama cha kikomunisti cha Urusi, Komredi Gennady Zyuganov ambae ni Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Urusi na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo alipomtembelea ofisini kwake. Mheshimiwa Spika yupo nchini humo akishiriki Mkutano wa 137 wa Chama cha Mabunge Duniani.


Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimkabidhi zawadi Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Urusi na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo Komredi Gennady Zyuganov (katikati) alipomtembelea ofisini kwake. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini huko, Jenerali Mstaafu Wynjones kisamba. Mheshimiwa Spika yupo nchini humo kushiriki mkutano wa 137 wa Chama cha Mabunge Duniani.

PICHA NA OFISI YA BUNGE

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents