Burudani

Picha: Tamasha la Muziki Mnene lafana Dar, Chidi apanda stejini na mabaunsa 3

Tamasha la Muziki Mnene linaloandaliwa na kituo cha redio na runinga cha EFM na ETV limefanyika kwa mafanikio katika Ukumbi wa Msasani Club Kinondoni jijini Dar es salaam.

Chidi Benz

Show hiyo ya aina yake iliyofanyika Jumamosi hii na kuwakutanisha wananchi wa aina mbalimbali lilikuwa na surprise kibalo iliwemo za wasanii.

Rapa Chidi Benz ndiye aliyefunga show hiyo kwa shangwe kubwa baada ya kutanguliwa na wasanii mbalimbali akiwemo, Izzo Bizness, Nuh Mziwanda, Kayumba, Madada Sita, Nedy Muziki pamoja na wasanii wengi wa singeli.

Chidi alipanda kwenye steji hiyo huku akiwa tofauti kidogo ambapo katika show hiyo alipanda na mabaunsa watatu waliokuwa wakimlinda hali ambayo ilisababisha msisimko wa aina yake ikiwa ni wiki chache toka atangaze kufanya kobalo na marehemu 2 Pac.

DJ Ommy Crazy aibukia Muziki Mnene wa EFM.

Kama nilivyokwambia usiku huo ulikuwa na surprise mbalimbali ukiacha na ile ya Chidi Benz kupanda na mabaunsa watatu, DJ Ommy Crazy ambaye kipindi cha nyuma alikuwa EATV NA EA Radio aliibukia katika tamasha hilo. DJ huyo kama kawaida yake alifanya yake katika ukumbi huo hali ambayo iliibua msisimko mkubwa.


Nuh Mziwanda

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents