Habari

Picha: Ufunguzi wa Olimpiki funika bovu!

Malkia Elizabeth wa Uingereza jana ameyafungua rasmi mashindano ya Olimpiki.
Ufunguzi huo umehusisha maceleb kibao wakiwemo David Beckham na Bradley Wiggins, pamoja ‘screen characters’ Mr Bean na James Bond.
Ukipewa jina la “Isle of Wonder, ufunguzi huo uliokuwa na ‘mbwembwe za kufa mtu’ uliongozwa na mshindi wa tuzo za Oscar aliyeongoza filamu maarufu za “Trainspotting” na “Slumdog Millionaire”, Danny Boyle.
Umehusisha ubunifu wa aina yake ulioangazia enzi za mapindiuzi ya viwanda hadi story ya James Bond, Harry Potter na Beatles, kama ishara ya Uingereza.
Steve Redgrave, aliyewahi kushinda medani za dhahabu mfululizo kuanzia mwaka 1984 hadi 2000, aliubeba mwenge wa Olimpiki kuuingiza uwanjani humo akiwa na wanamichezo saba vijana wa Uingereza.
Baadaye nyota wa kundi la Beatles, Paul McCartney alitumbuiza mbele ya umati wa watu 60,000 waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Olimpiki kwa kuimba wimbo “Hey Jude”.
Bingwa wa zamani ngumi wa uzito wa juu Muhammad Ali naye alionekana.
Kwa mujibu wa Reuters, zaidi ya watu bilioni moja duniani kote, walifungulia runinga zao kuangalia ufunguzi huo wa kihistoria.
Boyle alijikita katika enzi za mapinduzi ya viwanda nchini Uingereza katika karne ya 18 na 19, ambapo Uingereza ilijulikana kama ‘Karakana ya dunia’ ambapo mapinduzi hayo yaliubadilisha ulimwengu.
Hata hivyo kulikuwa na ufanano mkubwa kati ya ufunguzi huo wa London na ule wa mwaka 2008 wa Beijing Olympics.

Suala hilo limetokana na kuhusishwa kwa muongozaji wa filamu wa kichina Zhang Yimou, aliyedirect filamu ya mwaka 1991 ya “Raise the Red Lantern” na mpya zaidi ya “The Flowers of War,”ambaye alihusika pia na uaandaji wa sherehe za Beijing.
Ufunguzi huo umegharimu dola milioni 42 na umewakaribisha wanamichezo 16,000 kutoka nchi 204 duniani na huku wageni milioni 11 wakienda Uingereza kushuhudia mashindano hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents