Habari

Polisi waliomdhalilisha mchungaji wakufuzwa kazi

Askari polisi wanne mkoani Kilimanjaro waliotuhumiwa kutengeneza tukio la ushoga kwa mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania(KKKT) wamefukuzwa kazi.

Polisi hao walidaiwa kumkamata mchungaji huyo na mwanaume mwingine katika nyumba ya kulala wageni wilayani Hai, kumshurutisha avue nguo, kumpiga picha na kudai awalipe shilingi milioni 10 .

Hata hivyo mchungaji huyo ambaye jina lake limehifadhiwa aliwalipa shilingi 5.4 milioni polisi hao kumuachia baada ya kumshikilia kwa masaa sita.

BY: EMMY MWAIPOPO

CHANZO: MWANANCHI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents