Polisi wamuongezea ulinzi Rick Ross baada ya maisha yake kuwa hatarini tena

Rick Ross, rapper ambaye amekuwa akilengwa kushambuliwa na kundi la wahuni, ameongezewa ulinzi na polisi wa jijini New York, Marekani…. saa 24 kwasababu ya kupokea vitisho vingine.

Rick+Ross+Backstage+BET+Rip+Runway+Show+m6WNbNdVxn7l

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, polisi wamekuwa wakimlinda Ross aliyefikia kwenye hoteli ya The London kwa siku za hivi karibuni. Vyanzo vimeuambia mtandao huo kuwa vitisho vipya dhidi ya rapper huyo mwenye makazi yake jijini Miami, Florida hajavichukulia kawaida.

Mwezi uliopita Ross akiwa anaendesha gari lake aina ya Rolls-Royce alinusurika kupigwa risasi huko Ft. Lauderdale muda mfupi baada ya kutoka kwenye party ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Hata hivyo yeye na msichana aliyekuwa naye hawakujeruhiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents