Burudani

Prezzo na Goldie kupiga tour ya Africa?


Well, inafahamika kuwa mwakilishi wa mwisho kutoka Nigeria aliyeyaaga mashindano ya Big Brother Africa ni Goldie. Kwa muda wote aliokuwemo mjengoni humo alikuwa karibu sana na mfalme wa ‘pamba’ wa Kenya Prezzo kiasi cha kuwa wote kama kumbi kumbi.
Pamoja na kumuumiza mara nyingi mno, Goldie bado hajamsahau Prezzo na huenda wanamuziki hao wakakutana siku si nyingi zijazo na kupiga collabo huku ukiwepo uwezakano wa kufanyika tour ya pamoja barani Africa, how sweet is that!
Akiongea kwa simu na gazeti la The Star la Kenya, Goldie amesema: “Kabla sijaja mjengoni, nilikuwa nimeanza ziara ya kitaifa nchini Nigeria na wakati nikiwa kwenye BBA uongozi wangu uliachia single yangu mpya na video. Hivyo kwakuwa sasa nimetoka nitarejea kwenye ziara ya chuo kikuu ambayo nilianza na niimalize. Pia napanga kujitanua zaidi na kufanya tour barani Africa.”
Mrembo huyo pia alidokeza mipango ya collabo na Prezzo, “tuliongea muda wote tulipokuwa mjengoni. Nategema kuona jinsi hilo litakavyokuwa.”
Pia alisema anamtakia kila lakheri Prezzo kwenye kinyang’anyiro hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents