Habari

Private plate number ya milioni 5 kwenye gari ya milioni 8 inaingia akilini?

Unataka kuweka jina lako, la mwanao ama la kibanda chako kwenye plate number ya gari lako? Ni hela yako tu, milioni tano kwa miaka mitatu, mtaani watalijua jina lako. Katika pita pita yetu kwenye mitandao ya kijamii tumekutana na kali hii iliyoandikwa na mdau mmoja, anasema:

“Nimekutana na gari aina ya Toyota Premio ina hizi new plate numbers scheme iliyoanzishwa na TRA. Najua kuwa ni haki ya kila mtu kuamua kutupia hizi private number ila kama kawaida nikaingiwa na ushawishi wa haka kaugonjwa kangu kapya ka KUKOKOTOA…. hizi plate number ni 5m kwa miaka mitatu….hivi bei ya premio ni sh ngapi wadau kabla sijamaliza KOKOTO langu hili na ku conclude?”

Toyota Premio inauzwaje? Mdau mwingine akafunguka, “show room milioni 11, mkononi ikiwa imesimama saba, nane..”

Then tufanye mtu huyo aliinunua gari yake show room kwahiyo milioni 11, halafu ujiulize inaingia akilini kutumia shilingi milioni tano kuweka private plate namba kwenye gari ya bei hiyo?

Hii ni sawa na kuweka kiyoyozi kwenye nyumba ya nyasi sio?

“Nchi hii lolote linawezekana..unaweza kuta huyo mtu hajalipia hata hiyo 5M. Dar paogope sana..mambo ya private number yatachochea ujambazi,” alichangia mwingine.

Lakini wengine wanasema hiyo ni haki ya kila mtu na kama anaweza kumudu mwaache ajimwaye mwaye, “ila mtu ana uhuru wa kufanya atakalo ilimradi tu havunji sheria. Ku spend 30% ya gharama ya gari kwa ku enjoy plate number kuna ubaya gani ka mtu anaweza?.. si lazIma uspend 50m ndo uwe na “designers” number plate… Ntaweka soon kwenye Vitz….kitu gani bana? Unakunywa bia na bata nyingine kwa over 30% of your net income… kila mwezi… nothing strange to me.”

Really?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents