Burudani ya Michezo Live

Profesa J, MwanaFA, Chege, Roma na Ditto wajadili jinsi ya kuzuia uuzaji wa nyimbo zao mitaani

BURN CD

Kwa muda wa saa zaidi ya nne leo, wasanii kadhaa wa Bongo Flava na wadau wa muziki walikuwa wakijadili kwenye mtandao wa Twitter tatizo sugu la uuzwaji wa kazi zao mitaani (kuburn cd). Mjadala huo ulianzishwa na Profesa Jay aliyeanza kwa kutweet:

Roho inaniuma sana nikiona sehemu imeandikwa, TUNABURN BONGO FLAVA HAPA, TUNAWEKA KWENYE FLASH, KWA BLUTOOTH PIA.. Hivi kweli TUMESHINDWA??

Tweet hiyo ilivuta attention ya wasanii wengi na wadau wa muziki wakiwemo MwanaFA, Chege, Roma na Ditto:
Hivi ndivyo walivyojadili:

MwanaFA: @Profesa_Jay ndio inavyoelekea…tumeshindwa…ishakuwa kitu cha kawaida kabisa..tutakufa hatujafaidika na huu mziki…

Profesa: @MwanaFA unadhani tukijipanga upya kwa dhati kabisa hatutafanikiwa? TUANZIE WAPI?

MwanaFA: @Profesa_Jay natamani tungekuwa hatukuwahi kujaribu,pengine ningekuwa na moyo bado..unajua watu wetu walivyo..binafsi kama nimechemsha hivi

Profesa: @MwanaFA sawa sawa ngoja tuone labda tutakutia tena moyo urudi kundini maana nguvu yako na uwezo mkubwa wako ni muhimu sana kwa hili jambo!

Roma: @MwanaFA @Profesa_Jay KULIFANYA TATIZO LIISHE KABISA NI VIGUMU LAKINI UNAWEZA KULIPUNGUZA

Profesa:@Roma_Mkatoliki @MwanaFA @Profesa_Jay na hilo ndilo linalotakiwa haswa maana piracy ipo dunia nzima ila hapa imepitiliza!

MwanaFA: @Profesa_Jay @Roma_Mkatoliki yeah,ikipungua tu itasaidia..ipungue kwa kiwango kikubwa..kwisha kabisa haiwezekani

Ditto: @Profesa_Jay Mafanikio kwenye kukomesha hilo Upo kwenye mikono yetu wenyewe.

Roma: @Lameckditto @Profesa_Jay hivi kuna uwezekano bongo movie wana umoja sana kuliko sisi? na chama/club yao ipo active?

Chege: @Profesa_Jay hakuna kinacho shindikana chini ya jua mwamba,huo mchakato haujatolewa macho tu na serikali yetu,inauma sana kiukweli, eti imekua kitu cha kawaida tu ukitoa vieo mpya kesho unakuta inauzwa ubungo mataa!

Profesa: @ChegeChigunda Jamaa wanaona kama ni haki yao ya msingi hivi kuwanyonya wasanii we ngoja tuu SIKU ZAO ZINAHESABIKA…. NYAMBAAAAAAF

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW