Burudani

Profesa Jay na Times FM kusaidia wasiojiweza kwa ‘Nishike Mkono Tour’

Nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Joseph Haule aka Profesa Jay na kituo cha radio cha Times FM, wameandaa tour iliyopewa jina la ‘Nishike Mkono’ ili kuisaidia jamii katika masuala ya elimu na afya.

“Kwa jina naitwa Joseph Haule aka Profesa Jay mwanamuziki bora kabisa wa muziki wa kizazi kipya nimefanya muziki huu kwa muda mrefu nikiwa mmoja kati ya wasanii waliofanya mapinduzi makubwa kwenye muziki huu wa Bongo Flava nawashukuru sana mashabiki wangi kwa kunisupport kwa muda wote huo ambao nimefanya muziki huu hapa Tanzania na nje ya Tanzania na naamini siwezi kuwa Profesa Jay bila mashabiki wangu na kuzingatia hilo na kuona umuhimu wake niliamua kuanzisha kitu kinaitwa Profesa Jay Foundation For Tanzania Community nikiwa kama njia ya kuwaambia mashabiki wangu asanteni kwa kunishika mkono siku zote asanteni kwa kunisupport mpaka nilipofika hapa,” anasikika Mchawi huyo wa rhymes kwenye tangazo.

Tour hiyo itaanza October 26 katika maeneo ya Kibaha Kontena na October 27 CHEM CHEM – MLANDIZI.

Profesa ataambatana na wasanii kama JUMA NATURE, SUGU, AY, FA, AFANDE SELE, MADEE, NEY WA MITEGO, LINEX,BLACK RHYNO, BARNABA,MATONYA, SQUEEZER, MBATIZAJI na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents