Burudani

Pusha T akatisha Show yake Canada baada ya fujo kutokea, zahusishwa na bifu lake na Drake (+Video)

Pusha T akatisha Show yake Canada baada ya fujo kutokea, zahusishwa na bifu lake na Drake (+Video)

Usiku wa kuamkia leo rapper kutoka Marekani Terrence LeVarr Thornton kwa jina maarufu Pusha T, ameamua kukatisha show yake baada ya kutoke fujo.

Rapper huyo alikuwa akitumbuiza kwenye mji wa Toronto nchini Canada, ambapo ghafla jukwaa lilianza kushambuliwa kwa kurushiwa pombe na wengine kuvamia jukwaa wakitaka kumdhuru. Polisi wameripoti kuwa ilimlazimu Pusha aikatishe show yake.

Sababu kubwa kabisa ya vurugu hizo ni kuhusu lile bifu lake kubwa na mwanamuziki kutoka Canada na hasa katika jiji la Toronto ambaye ndio makazi ya Drake, kwahiyo waliovamia show hiyo wakidaiwa ni mashabiki wa Drake kutokana na bifu lao ambalo ni kubwa sana.

Wengine wakienda mbali zaidi wakisema fujo hizo yeye Pusha T alijitakia kwani alijua fika huko ndio ngome ya Drake lakini akajitoa ufahamu na kwenda kupiga show Toronto.

Watu kadhaa wameripotiwa kuumizwa huku Pusha akitoka salama. Show hiyo ambayo ni muendelezo wa ziara yake ‘The Daytona Tour’ ilikuwa SOLD OUT mwezi mmoja kabla. Toronto ni ngome ya Drake ambaye wana bifu kwa miaka kadhaa sasa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents