Burudani

Q chief awatolea uvivu wasanii wanaotoa ngoma nyingi kwa muda mfupi

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Q chief amewatolea uvivu wasanii wanaotoa nyimbo nyingi kwa muda mfupi kwa kusema hawajiamini ndio maana wanaachia nyimbo nyingi kwa muda mfupi.

Q Chief

Q Chief amesema kama msanii anafanya muziki unaodumu kama yeye haina haja ya kutoa nyimbo nyingi mfululizo kwa muda mfupi huku akidai wasanii wanaofanya muziki wa Big G au ‘Bubble Gum’ ndio wanaohangaika kutoa nyimbo kila siku.

“Naamini kabisa mimi ni mgodi unaotembea, naogopa ninapoona ngoma inaHit siku mbili na kupotea, nia yangu ni kufanya muziki ambao utaishi hata nikiondoka… mimi nadhani wanaotoa ngoma nyingi kwa muda mfupi bila mpangilio ni waoga, hawajiamini ndiyo maana wanahangaika na ngoma kila kukicha kama unafanya muziki unaodumu haina haja”,amesema QChief kwenye mahojiano yake na kituo cha radio cha EFM.

Hata hivyo Q Chief amesema muziki wetu unapoteza ladha yake asili kila kukicha kutokana na wasanii kujikita kuiga aina nyingine ya miziki kutoka nje.

“Nafurahi kuona wadogo zangu wanapeleka Bongo fleva Mbele lakini nikiingalia Bongo Fleva naona kabisa tunahama kwenye misingi yetu na hii inatokana na baadhi yao wanaopata nafasi ya kwenda mbele sio wasanii ndio maana wanapokutana na wasanii wenye uwezo wanaruhusu Identity ya Bongo Fleva ipotee na kuanza kuwaiga”,amesema Q Chief.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents