Raila Odinga azidi kuwaweka karibu mastaa wa Kenya

Waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga ameamua kujiweka karibu zaidi na wasanii maarufu nchini ambao huenda wakamsaidia kwenye kampeni za uchaguzi ujao nchini humo.

Baada ya kukutana na Prezzo na Jaguar mwezi uliopita, waziri huyo mkuu hivi karibuni amekutana pia na staa wa dancehall nchini humo,Redsun.

Haijulikani ni nini ambacho huzungumzwa kwenye mikutano hiyo, lakini wengi wanaamini kuwa huenda akawatumia wasanii hao kwenye kampeni yake ya urais wa Kenya.

Tayari kuna tetesi kuwa wanasiasa kadhaa wanafanya mazungumzo na Jaguar ili wautumie wimbo wake uitwao ‘Matapeli’ kwenye kampeni zao na huenda Raila Odinga akawa ni mmoja wao.

Uchaguzi wa urais nchini Kenya utafanyika mwezi March, 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents