Habari

Raila Odinga hatokubali kushindwa uchaguzi, ajipanga kwenda kortini kama Kenyatta akitangazwa mshindi

Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amedaiwa kuwa hatokubali kushindwa katika uchaguzi wa urais wa wiki hii na ataanzisha harakati za kisheria kama mpinzani wake Uhuru Kenyatta atatangazwa rasmi kuwa Rais leo.

raila

Kambi ya Odinga ilidai zoezi la kuhesabu kura lilikumbwa na kasoro kibao na alitaka lisimamishwe.

“Hatokubali kushindwa uchaguzi. Kama Uhuru Kenyatta akitangazwa kuwa Rais mteule ataenda mahakamani mara moja,” mshauri wa karibu wa Odinga Salim Lone, ameliambia shirika la habari la Reuters.

Mpaka sasa Kenyatta anayewakilisha muungano wa Jubilee amepata kura 6,173,433 huku Odinga akiwa na kura 5,340,546 kati ya kura 12,221,053 zilizopigwa na hivyo Uhuru kufanikiwa kuvuka kigezo cha asilimia 50 na kura moja na kumpa ushindi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents