Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Rais Dkt. Magufuli ampongeza Uhuru Kenyetta

Baada ya leo Uhuru Kenyatta kutangazwa ndiye mshindi wa kiti cha urais kwa mara nyingine tena nchini Kenya kufuatia uchaguzi uliofanyika August 8 mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amempongeza Uhuru kwa ushindi huo.

Rais Dkt. Magufuli ametuma salamu hizo za pongezi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter na kumtakiwa Uhuru mafanikio katika kutumikia wananchi waliomchagua.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi na Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) kwa kupata kura 8, 203, 290 sawa na asilimia 54.2, huku mgombea wa upinzani Raila Odinga akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.7.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW