Burudani ya Michezo Live

Rais Magufuli aagiza Kampuni ya Barrick Gold, kuyachukua Makontena ya Makinikia yaliyozuiliwa bandarini ili wayauze – Video

Rais Magufuli aagiza Kampuni ya Barrick Gold, kuyachukua Makontena ya Makinikia yaliyozuiliwa bandarini ili wayauze - Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ameiagiza Kampuni ya Barrick Gold, kuyachukua yale Makontena ya Makinikia yaliyozuiliwa bandarini ili wayauze kwa faida ya kampuni ya Twiga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Hayo ameyabainisha leo Januari 24, 2020, Ikulu ya Jijini Dar es Salaama mara baada ya kushuhudia utiaji wa saini wa makubaliano ya mikataba Tisa ya Madini kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick Gold, ambapo kwa pamoja wameingia makubaliano ya kuunda Kampuni ya Twiga itakayokuwa ikisimamia Madini.

“Yale Makontena ambayo yako bandarini, ambayo tuliyashika sasa mkatafute wabia mkayauze  kwa faida ya kampuni ya Twiga, today is a new page, is a new life” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi ameeleza ni kwa namna gani alikutana na ugumu na changamoto kubwa wakati wa mchakato huo na kuomba msamaha kwa chochote ambacho kitakuwa kimepungua kutokana na mikataba hiyo.

“Naomba niombe msamaha kwako na kwa Watanzania wote kwa lolote litakalokuwa limepungua, limetokana na ubinadamu wetu na muwe na uhakika, tulifanya kazi hii kwa moyo wetu wote, akili zetu zote na nguvu zetu zote” amesema Waziri Kabudi.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW