Habari

Rais Magufuli aitaka TBC kutangaza habari bila kubagua vyama

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amelitaka shirika la utangazaji la TBC, kutoa taarifa kwa Watanzania bila kujali chama wala bila kubagua kabila.

Rais Magufuli ameyasema hayo katika ofisi za shirika hilo huku akilitaka liwe shirika la kwanza kuhabarisha jamii.

“Msemaji wa Serikali mkubwa ni TBC1 na Redio ya Taifa, nyinyi hamuwezi mkawa kama vyombo vingine ambavyo vina malengo yao ya kufanya biashara, nyinyi kazi yenu ni kutoa taarifa sahihi kwa Watanzania bila kubagua vyama vyao, bila kubagua dini zao, bila kubagua makabila yao, huo ndio uwe msimamo mkuu.

Rais Magufuli jana alifanya ziara katika ofisi hizo na kuzungumza na wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na kujua changamoto zinalolikabili shirika hilo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents