Habari

Rais Magufuli ametuvunia wanachama wapya milioni sita CCM – Humphrey Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa Mwaka 2015 chama hicho kilifanya utafiti wa wananchama wao.

Polepole ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa Ripoti ya pili Twaweza kuhusiana na tafiti zake kuhusu maoni ya wananchi wa Tanzania kuhusu Ushiriki, Maandamano na Siasa kwa mwaka 2018

Polepole amesema kuwa mwaka 2015 walikuwa na wananchama milioni nane na laki nne mpaka mwaka 2017 wananchama waliongezeka na kuwa milioni 13 wenye kadi mkononi.

“Mwaka 2015, tulifanya utafiti wa wanachama wetu, tulikua nao milioni 8 na laki 4. Mwaka 2017 tuliongezeka mpaka milioni 13 wenye kadi na wamezishika mkonononi. Kwa kipindi cha miaka 2 ya Rais Magufuli ametuvunia wanachama wapya zaidi ya milioni 6. Hii tafsiri yake ni nini? Ni kwamba 2020 tukishinda kwa asilimia 80 msishangae,” amesema Polepole.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents