Habari

Rais Magufuli ashinda kura 100% kuiongoza CCM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, huku Rais Shein akwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar.

Rais Magufuli ameshinda nafasi hiyo leo, baada ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama hicho kumpitisha kwa kura zote 1821 mjini Dodoma wakati Mkutano Mkuu wa 9 wa Chama hicho ukiendelea.

Kura zilizopigwa ni 1821, Halali-1821, Zilizoharibika- 0, Hapana-0, Ndiyo-1821.

Hata hivyo wakati Rais Magufuli akipigiwa kura, aliteuliwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini William Mkapa kuwa Mwenyekiti wa muda kuongoza zoezi hilo la upigaji kura.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents