Habari

Rais Magufuli atembelea shule aliyosoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika shule ya msingi Chato alikosoma darasa la kwanza hadi la saba na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, ilieleza kuwa Rais alifanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo.

Akizungumza na wanafunzi shuleni hapo, Magufuli aliwaasa kutilia mkazo masomo ili waweze kufaulu na kuwataka walimu kuhakikisha wanatumia vyema fedha zinazotolewa na serikali kila mwezi za elimu bila malipo na pasiwe na wanafunzi hewa.

Rais alisema yapo maeneo na shule mbalimbali nchini kumebainika kuwa na wanafunzi hewa katika uhakiki unaofanywa na serikali na kuwaasa shule hiyo kuwa wasiwe kama shule hizo huku akitaka wanafunzi shuleni hapo pia wahakikishe hakuna wanafunzi hewa.

Kwa upende wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi hiyo, Mwita Chacha alimshukuru Rais Magufuli kwa msaada aliowapatia katika kukabiliana na uhaba wa madarasa uliokuwa unaikumba shule hiyo, pia kuitembelea shule yao jambo ambalo limewatia moyo walimu na wanafunzi shuleni hapo.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents