Habari

Rais Magufuli ‘awapiga stop’ viongozi kuhudhuria sherehe za kilele cha Mwenge wa Uhuru

Taarifa iliyotolewa Jumatano hii na Ikulu ya Dar es Salaam, imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zitakazofanyika Oktoba 14, wilayani Bariadi, kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho za safari wazirejeshe.

magu1-1

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi katika shughuli za maendeleo ya nchi.

Viongozi waliotajwa kutakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na Wakuu wote wa Mikoa, Wakuu wote wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mameya na Wenyeviti wote wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo madereva na wasaidizi wao ambao kwa idadi hufikia takribani 1,500.

Kwakuwa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru huambatana na Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia miaka 17 iliyopita, agizo hilo limewataka viongozi wote wa mikoa na wilaya kubaki katika maeneo yao ya kazi na kujiwekea utaratibu wa jinsi ya kuienzi siku hiyo.

Mgeni rasmi katika sherehe za kuzima mwenge wa Uhuru atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

1945affc-5580-4375-9341-ba05030514bc

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents