Habari

Rais Magufuli awataka TAKUKURU kufanya kazi kwa weledi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU kufanya kazi kwa kuzingatia uweledi, Uzalendo na Uadilifu mkubwa na kwamba serikali itafanyia kazi changamoto zinazowakabili.

 

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa TAKUKURU katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo Rais Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale
wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

“Kuna mambo mengi ya hovyo yanafanyika, tumehakiki pembejeo za ruzuku na kubaini madai ya Shilingi Bilioni 48 ni hewa, tumebaini wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, tumebaini kaya masikini hewa 56,000 zilizopaswa kupata fedha TASAF, tumebaini wanafunzi hewa 5,850 waliotakiwa kupata mkopo, kuna vichwa vya treni 11 vimeletwa  bila kuwepo mkataba na mengine mengi, haya yote yanafanyika kwa rushwa, nataka kuwaona mnachukua hatua stahiki” alisema Rais Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents