Rais Magufuli Punda afe mzigo ufike – Afande Sele

Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitoa hotuba kwa viongozi mbalimbali aliowaapisha siku hiyo, kuna baadhi ya maneno aliyoyasema ndani ya hotuba yake yalikuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo katika hotuba yake,Rapa mkongwe nchini Tanzania, Afande Sele hakutaka kukaa nyuma aliguswa na kuamua kuchukua baadhi ya maneno aliyoyazungumza Rais Magufuli na kuyaweka katika mtandao wake wa Instagram. Afande ameandika “Dume La Simbaaaaa….Gusa Unase….Maendeleo sio lele mama ni kauli ya baba wa taifa mwlm Nyerere…No pain No gain…Punda afe mzigo ufike…ukicheka na nyani utavuna mabua…Ngosha kanyaga twende kama china kama North korea hadi kieleweke…muda wa kucheka na kuku ulishapita sasa kazi tuu…..Chuma kikoli moto….”

Utakumbuka Marchi 15, 2018, Afande Sele alingaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi mkoani Morogoro mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Pia Afande Sele kabla ya kujiunga na CCM alishawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na Chama cha ACT Wazalendo ambapo mwaka 2015 alitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW