Habari

Rais wa zamani wa Botswana afariki dunia

Serikali ya Botswana imetangaza kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Sir Ketumile Masire amefariki dunia usiku wa kuamia jana.

 

Taarifa ya kifo cha kiongozi huyo iliwekewa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, iliandikwa “Hii ni kuthibitishwa kwamba mpendwa wetu Rais wa zamani  Sir Ketumile Quett Joni Masire amefariki dunia, Roho yake ipumzike amina.”

Rais huyo alikuwa na miaka 91 ameliongoza taifa hilo kuanzia mwala 1980 hadi 1998 atakumbukwa kwa jinsi alivyoweza kuimarisha utulivu na amani paoja na kujenga misingi bora ya mafanikio kiuchumi.

Kwa upande wa Balozi wa Afrika Kusini nhini . Mdu Lembede amekaririwa na Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) akisema rais huyo aliweza kuunga mkono harakati za taifa lao la kupambana dhidi ya utawala wa kibaguzi pia alishiriki katika harakati za ukombozi ktika nchi za Afrika kama vile Namibia, Zimbabwe na Msumbiji.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents