Habari

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amtimua waziri wa Nishati, kwa sababu ya tatizo la kukatika umeme mara kwa mara

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amtimua waziri wa Nishati, kwa sababu ya tatizo la kukatika umeme mara kwa mara

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amemfukuza kazi waziri wa nishati, Joram Gumbo kwa sababu ya tatizo la kukatika umeme mara kwa mara tangu mwaka 2016. Nafasi ya waziri huyo amepewa naibu waziri wa usafirishaji na miundo mbinu Forune Chasi. Gumbo sasa amepewa wadhifa wa kuwa waziri katika ofisi ya rais ,kufuatilia utendaji na utekelezaji wa idara za serikali.

Kwa mujibu wa BBC. Kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali amesema siku ya jumatatu kuwa umeme ambao umekuwa ukikatika kwa saa tano au nane kutokana na upungufu wa maji katika mtambo mkubwa wa uzalishaji umeme. Siku ya jumatatu , kampuni ya uzalishaji umeme inayomilikiwa na serikali ilitangaza kuwa umeme utakatika kwa saa tano mpaka nane. Vilevile machimbo ya migodi yatahathirika na kukatika huko kwa umeme.

Mamlaka inalaumu kuzimika au kukatika kwa umeme huo kutokana na mtambo wa uzalishaji umeme kuzalisha umeme kwa kiwango kidogo kutokana na ukame ambao umesababisha maji kupatikana kwa kiwango kidogo. Baadhi ya nchi jirani wamedai kuwa umeme kwao umewahi kukatika kwa muda mrefu zaidi hadi saa 10. Aidha serikali ya Zimbabwe imepanga kuagiza nishati kutoka nchi jirani ya Msumbiji na Afrika kusini.

Kabla ya mwaka 2016, tatizo hilo la umeme limezua gumzo katika mitandao ya kijamii tangu wakati huo mpaka sasa .Awali raia wengi wa Zimbabwe walikuwa wanawaonea huruma majirani zao wa Afrika Kusini kwa kukatikiwa umeme mara kwa mara lakini sasa tatizo limerudi kwao.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents